Picha : BASI LA ALLYS LAPINDUKA, LAUA NA KUJERUHI WATU 25 SHINYANGA
Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Lucas Maganga (25) mkazi wa Shinyanga mjini amefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya Basi la Allys lenye namba za usajili T. 979 CDH lililokuwa linatoka Ushirombo kwenda Bariadi mkoani Simiyu kupasuka gurudumu na kupinduka eneo la Maganzo mkoani Shinyanga. Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Septemba 25,2017 majira ya saa nne asubuhi. Mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia Malunde1 blog kuwa gurudumu la mbele la basi hilo lilipasuka na kwamba dereva wake Salumu Mseke alikuwa akiendesha kwa mkono mmoja huku akiongea na simu ya mkononi. Wamesema basi hilo lina uwezo wa kubeba abiria 50,lakini waliokuwa ndani ya basi ni zaidi ya 70 na dereva alikimbia baada ya kusababisha ajali hiyo. Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Basi la Allys Sports likiwa kimepinduka Tairi likiwa limepasuka Uokoaji ukiendelea