Picha : BASI LA ALLYS LAPINDUKA, LAUA NA KUJERUHI WATU 25 SHINYANGA
Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Lucas Maganga (25) mkazi wa
Shinyanga mjini amefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya Basi la
Allys lenye namba za usajili T. 979 CDH lililokuwa linatoka Ushirombo
kwenda Bariadi mkoani Simiyu kupasuka gurudumu na kupinduka eneo la
Maganzo mkoani Shinyanga.
Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Septemba 25,2017 majira ya saa nne asubuhi.
Mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia Malunde1 blog kuwa gurudumu la mbele
la basi hilo lilipasuka na kwamba dereva wake Salumu Mseke alikuwa
akiendesha kwa mkono mmoja huku akiongea na simu ya mkononi.
Wamesema basi hilo lina uwezo wa kubeba abiria 50,lakini waliokuwa ndani
ya basi ni zaidi ya 70 na dereva alikimbia baada ya kusababisha ajali
hiyo.
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Basi la Allys Sports likiwa kimepinduka
Tairi likiwa limepasuka
Uokoaji ukiendelea
Maoni
Chapisha Maoni