JPM amwaga ajira 3,000 JWTZ



Rais John Magufuli ametangaza kutoa nafasi 3,000 kwa vijana waliopitia mafunzo ya ukakamavu kujiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
Akizungumza baada ya kuwatunuku nishani ya Luteni Usu maofisa 422 wa jeshi, Magufuli amesema lengo la kutoa nafasi hizo ni kuhakikisha jeshi linakuwa na askari wa kutosha.
“Jeshi haliwezi kuwa na maofisa tu, tutaongeza na askari wa kawaida, wengi watakaopata nafasi hizi nataka wawe wamepitia JKT, tunataka tujenge jeshi la kisasa.”
Rais Magufuli amewataka Watanzania kutoa ushirikiano kwa jeshi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili viendelee kufanya kazi yao kwa ufanisi, amani na utulivu viendelee kutawala nchini.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HUYU NDIO DJ MARK WA 92.2FM SUMBAWANGA.....