MAGUFULI KUONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA - NEC KWA SIKU MBILI DAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), Taifa, anatarajia kuongoza kikao cha Halmashauri Kuu
ya Taifa (NEC) kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam, Septemba 30 hadi
Oktoba 1, 2017.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana
Septemba 24 na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole
ameeleza kuwa, Kamati kuu ya Halmashauri ya Taifa (CC) na Halmashauri
Kuu ya Taifa (NEC) vinatarajia kuketi Jijini Dar e Salaam kwa nyakati
tofauti.
Maoni
Chapisha Maoni