MBUNGE MSIGWA KURIPOTI POLISI LEO BAADA YA KUACHIWA KWA DHAMANA JANA USIKU
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Peter
Msigwa ameachiwa huru jana usiku kwa dhamana baada ya kukamatwa akiwa
kwenye mkutano wa hadhara.
Msigwa aliachiwa baada ya kudhaminiwa na
wadhamini wawili Alex Kimbe pamoja na Mwenyekiti wa Bavicha Iringa
Leonce Marto , saa nne usiku .
Msigwa alishushwa jukwaani kwa nguvu
akiwa anahutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Mlandege Manispaa ya
Iringa na anatuhumiwa kwa kosa la uchochezi dhidi ya vyombo vya usalama .
Marto amesema mikutano yake imefungiwa
na hapaswi kuendelea na ziara yake katika kata nyingine mpaka hapo OCD
atakapo amua vinginevyo.
Leo Mbunge anatakiwa kuripoti kwa RCO
na huenda kesi ya uchochezi ambayo tayari imeshafunguliwa jalada lake
ikapelekwa mahakamani .
Amesema Mbunge huyo atazungumza na
vyombo vya habari leo mchana kuweka wazi madhila yaliyompata wakati
akitekeleza wajibu wake kwa wananchi.
Maoni
Chapisha Maoni