Diamond atua Afrika Kusini kwa Zari


Ikiwa zimepita siku nne tangu mwanamuziki Diamond Platnumz akiri kumsaliti mpenzi wake Zari, hatimaye ametua nyumbani kwa mwanamke huyo nchini Afrika Kusini.
 Leo saa 5.40 asubuhi mwanamuziki huyo aliposti video katika mtandao inayomuonyesha akicheza na mtoto wake wa kwanza, Latifah huku kwa mbali ikisikika sauti ya Zari.
Dada wa mwanamuziki huyo, Esmah Khan aliposti video hiyo katika mtandao wa Instagram: “Tuko na Tiffah na mamy tunaita raha ya mtoto apewe mapenzi kwa baba na mama jamani.” 
Leo ilikuwa siku muhimu kwa Zari kwani anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HUYU NDIO DJ MARK WA 92.2FM SUMBAWANGA.....