Machapisho

Picha : BASI LA ALLYS LAPINDUKA, LAUA NA KUJERUHI WATU 25 SHINYANGA

Picha
Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Lucas Maganga (25) mkazi wa Shinyanga mjini amefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya Basi la Allys lenye namba za usajili T. 979 CDH lililokuwa linatoka Ushirombo kwenda Bariadi mkoani Simiyu kupasuka gurudumu na kupinduka eneo la Maganzo mkoani Shinyanga.  Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Septemba 25,2017 majira ya saa nne asubuhi.  Mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia Malunde1 blog kuwa gurudumu la mbele la basi hilo lilipasuka na kwamba dereva wake Salumu Mseke alikuwa akiendesha kwa mkono mmoja huku akiongea na simu ya mkononi. Wamesema basi hilo lina uwezo wa kubeba abiria 50,lakini waliokuwa ndani ya basi ni zaidi ya 70 na dereva alikimbia baada ya kusababisha ajali hiyo. Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.  Basi la Allys Sports likiwa kimepinduka Tairi likiwa limepasuka Uokoaji ukiendelea

MAGUFULI KUONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA - NEC KWA SIKU MBILI DAR

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Taifa, anatarajia kuongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam, Septemba 30 hadi Oktoba 1, 2017. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Septemba 24 na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole ameeleza kuwa, Kamati kuu ya Halmashauri ya Taifa (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) vinatarajia kuketi Jijini Dar e Salaam kwa nyakati tofauti.

MBUNGE WA CHADEMA JOSHUA NASSARI "NIPO TAYARI KUJIUZULU UBUNGE..NINA USHAHIDI MADIWANI KUPEWA RUSHWA KUJIUZULU"

Picha
Mbunge wa Chadema wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ameweka rehani ubunge wake  baada ya Rais John Magufuli kumpokea aliyekuwa diwani wa chama hicho aliyejiuzulu akisema ni kwa sababu ya kuunga mkono juhudi za Rais. Nassari amedai ana ushahidi wa kielektroniki unaoonyesha madiwani hao walivyopewa rushwa ili wajiuzulu nafasi zao. Hata hivyo, diwani wa Kata ya Kimandolu, Mchungaji Rayson Ngowi ambaye amepokewa na Rais Magufuli juzi  baada ya kujiuzulu Chadema akizungumzia tuhuma hizo alisema madai hayo hayana ukweli wowote na kama Nassari ana ushahidi ni vyema angeutoa hadharani. Ngowi aliwashauri Chadema mkoani Arusha watatue matatizo yaliyopo ndani ya chama hicho na wasitafute visingizio kwa kuwa yeye ameamua kujiuzulu kwa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli na hajapewa rushwa yoyote. Diwani mwingine aliyejiengua katika chama hicho wa Kata ya Muriet, Credo Kifukwe alisema hakuna chochote alichopewa kama rushwa kwa lengo la kujiuzulu, akims...

MBUNGE MSIGWA KURIPOTI POLISI LEO BAADA YA KUACHIWA KWA DHAMANA JANA USIKU

Picha
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Peter Msigwa ameachiwa huru jana usiku kwa dhamana baada ya kukamatwa akiwa kwenye mkutano wa hadhara. Msigwa aliachiwa baada ya kudhaminiwa na wadhamini wawili Alex Kimbe pamoja na Mwenyekiti wa Bavicha Iringa Leonce Marto , saa nne usiku . Msigwa alishushwa jukwaani kwa nguvu akiwa anahutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Mlandege Manispaa ya Iringa na anatuhumiwa kwa kosa la uchochezi dhidi ya vyombo vya usalama . Marto amesema mikutano yake imefungiwa na hapaswi kuendelea na ziara yake katika kata nyingine mpaka hapo OCD atakapo amua vinginevyo. Leo Mbunge anatakiwa kuripoti kwa RCO na huenda kesi ya uchochezi ambayo tayari imeshafunguliwa jalada lake ikapelekwa mahakamani . Amesema Mbunge huyo atazungumza na vyombo vya habari leo mchana kuweka wazi madhila yaliyompata wakati akitekeleza wajibu wake kwa wananchi.

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 25,2017 -NDANI NA NJE YA TANZANIA

Picha
Magazetini leo Jumatatu Septemba 25,2017

MKE WA TUNDU LISSU AFUNGUKA KWA MARA KWANZA....DEREVA WA LISSU ASEMA HANA KUMBUKUMBU TUKIO LA KUPIGWA RISASI

Picha
Nairobi. Kwa mara ya kwanza, Alicia Magabe ambaye ni mke wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia tukio la mumewe kushambuliwa kwa risasi na kudokeza kwamba haliwezi kuwa limetokana na sababu nyingine isipokuwa kazi ambazo amekuwa akizifanya. Pia amezungumzia kuhusu afya yake na kueleza kuwa bado siyo nzuri na kuwaomba Watanzania waendelee kumuombea. Mbali ya Alicia ambaye pia ni mwanasheria, dereva wa Lissu naye amezungumza akisema ameathiriwa kwa kiasi kikubwa na tukio hilo huku akiahidi kuripoti polisi mara baada ya kurejea nchini. Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), amelazwa katika Hospitali ya Nairobi tangu alipopelekwa huko baada ya kupigwa risasi akiwa ndani ya gari nje ya nyumba yake mjini Dodoma mchana wa Septemba 7 akitokea bungeni. “Watanzania wote wanajua Lissu maisha yake yote amekuwa ni mtetezi wa wanyonge na tukio hili amelipata kutokana na kazi zake hizo hivyo nawaomba tumuombee tu,” alisem...

Diamond atua Afrika Kusini kwa Zari

Picha
Ikiwa zimepita siku nne tangu mwanamuziki Diamond Platnumz akiri kumsaliti mpenzi wake Zari, hatimaye ametua nyumbani kwa mwanamke huyo nchini Afrika Kusini.  Leo saa 5.40 asubuhi mwanamuziki huyo aliposti video katika mtandao inayomuonyesha  akicheza na mtoto  wake wa kwanza, Latifah huku kwa mbali ikisikika sauti ya Zari. Dada wa mwanamuziki huyo, Esmah Khan aliposti video hiyo katika mtandao wa Instagram: “Tuko na  Tiffah na mamy  tunaita raha ya mtoto apewe mapenzi kwa baba na mama jamani.”  Leo ilikuwa siku muhimu kwa  Zari kwani anasherehekea  siku yake ya kuzaliwa.