UNA TANZANIA YAZIJENGEA UWEZO ASASI ZA VIJANA ZA TANZANIA BARA NA VISIWANI


Mkufunzi Nuria Mshare akitoa mada kuhusu ushawishi na utetezi kwa maafisa miradi wa asasi za vijana kuhusu namna ya kufanya shughuli ushawishi, utetezi na ufuatiliaji wa haki za vijana katika ngazi ya serikali za mitaa, kitaifa na kimataifa kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Saddam Khalfan (Afisa wa Program - UNA Tanzania) akielezea kuhusu sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 na mchakato wa kupitia upya sera hiyo na mchakato wa kukusanya maoni ya sera ya maendeleo ya vijana kwenye mkutano uliowakutanisha asasi mbalimbali za vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society ili kuwajengea uwezo katika ushawishi na utetezi na ufuatiliaji wa haki za Vijana.
Rais Wa Chama ca Walimu wenye Uziwi(CWUT), Theresia Nkwera(kulia) akipata ufafanuzi wa mafunzo kwa vitendo kutoka kwa Bi Eliza William wakati wa uwasilishwaji wa mada kuhusu usashwishi na utetezi kwa maafisa miradi wa asasi za vijana kuhusu namna ya kichambua sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 na mchakato wa kupitia upya sera.


Baadhi ya maafisa miradi wa asasi za vijana wakichangia mada kuhusu sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 kwenye mkutano uliowakutanisha ili kujadili namna ya kufanya kazi kwa pamoja ili kuwa na sauti moja kwenye sera ya vijana. 



Baadhi ya maafisa miradi wa asasi za vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakifuatilia mada kuhusu sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 na mchakato wa kupitia upya sera hiyo na mchakato wa kukusanya maoni ya sera ya maendeleo ya vijana.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HUYU NDIO DJ MARK WA 92.2FM SUMBAWANGA.....