MWANAMKE WA AJABU 'ANAYEJISAIDIA OVYO KWENYE NYUMBA ZA WATU' ASAKWA NA POLISI
Polisi katika huko Colorado nchini Marekani wanamsaka mwanamke mkimbiaji ambaye amepewa jina la bandia kama "mchafuzi kichaa " - ambaye amekuwa akiendelea kujisaidia haja kubwa nje ya nyumba za watu.
Cathy Budde anase mwanamke huyo amekuwa akiacha kinyesi chake nje ya nyumba yake hadi mara saba kwa katika wiki za hivi karibuni ,licha ya kwamba kuna misalani ya umma karibu.
Anasema watoto wake walimuona mwanamke huyo wakati alipokuwa akijisaidia,akiwa amechuchumaa karibu na nyumba Colorado.
Idara ya polisi mjini humo imesema kuwa tabia ya aina hiyo ni ya "ajabu".
Kamanda wa polisi Luteni Howard Black ameiambia BBC kwamba mshukiwa anaweza kushtakiwa chini ya sheria inayopiga marufuku kujisaidia haja kubwa na ndogo kwenye maeneo ya umma.
" Sijawahi kukutana na kisa cha aina hii miaka 35 tangu kuanzishwa kwa idara hii ,"aliongeza.
Alisema kuwa haijabainika wazi kuwa tabia yake mwanamke huyo inatokana na matatizo ya kiakili au la.
Bi Budde alikiambia kituo cha habari cha KKTV kwamba aliwahi kumfokea mwanamke huyo
" Nilitoka nje siku moja nilipomuona , nikasema ni kweli unafanya hayo unayoyafanya ama naota?' Ni kweli unaleta kinyesi chako hapa mbele ya watoto wangu ?' alisema Yaa, samahani!'
" Kusema ukweli nilifikiri alikuwa na shida , ilikuwa ni bahati mbaya, Alienda akachukua mfuko , akasafisha na hakufanyia mazoezi ya kukimbia tena eneo hili."
Bi Budde aliongeza kusema kuwa: "tulimkamata tena mara nyingine mbili - tulpomkamata siku hiyo kesho yake akabadilisha muda kidogo wa kujisaidia kwasababu alifahamu nilikuwa ninamuona.
"niliweka kitu mfano wa ukuta, hii ilikuwa ni kama ishara ya kusema tafadhali, nakuomba ukome kufanya hicho unachokifanya.''
Lakini anasema hilo halikumzuwia mwanamke huyo anayefanya mazoezi ya kukimbia kujisaidia nje ya makazi ya Bi. Budde.
Chanzo-BBC
Maoni
Chapisha Maoni