Machapisho

DC MTANDA ASIKITISHWA NA CLOUDS MEDIA KUWADHALILISHA WALIMU WA KIKE NKASI.

Picha
Mkuu wa wilaya Nkasi Said Mtanda amehuzunishwa na kitendo cha Walimu wa kike kudhalilishwa kwa taarifa isiyokuwa na Ukweli. Hii inakuja baada ya Taarifa iliyotoka leo 11/03/2018 kupitia kurasa ya Kituo cha Matangazo cha CLOUDS iliyosomeka Kupitia Taarifa hiyo mkuu wa wilaya Nkasi Mh.Said Mtanda kupitia Ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa "Nimesikitishwa sana kwa taarifa hii

Ujenzi wa kituo cha Afya Kirando wapamba moto...

Picha
Mkuu wa wilaya Nkasi Mh.Said Mtanda amekagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya kirando kinachokadiriwa kukamilika kwa gharama ya Sh.milion700 ikiwa ni sambamba na Ununuzi wa Vifaa tiba.Katika ziara hiyo mkuu wa wilaya aliongozana na Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mh.Ally kessy kufuatilia hali ya ujenzi wa kituo hicho.Ikiwa ni siku chache zilizopita tangu wananchi wa mji wa Kirando wajitokeze kwenye Songambele ya Ujenzi wa kituo hicho katika hatua ya awali(msingi) ili kubana matumizi ya fedha na kuongeza jengo la kuhifadhia maiti.

UVCCM MKOA WA RUKWA WAADHIMISHA MAADHISHO YA SHEREHE ZA MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR KWA STYLE YA PEKEE,WAWATAKA WAPINZANI KUACHA KEJERI NA KELELE ZA CHURA MAJINI

Picha
Mwenyekiti Wa Vijana Wa CCM Mkoa Wa Rukwa Ndugu *Ramadhani Shabani* Leo Hii Ktk Maadhimisho Ya Mapinduzi Matukufu Ya Zanzibar Mkoani Rukwa Aliwaoongoza Vijana Wa CCM Mkoani Rukwa Kufanya Usafi Ktk Maeneo Ya Soko Kuu Ililopo Sabasaba Ambapo Pia Sambamba Na Yote Mwenyekiti Huyo Wa Vijana Pia Alisikiliza Kero Za Wafanyabiashara Ktk Soko Hilo. Mwenyekiti Huyo Wa Vijana Alisikiliza Kero Hizo Za Wafanyabiashara Hao Na Kuzipatia Ufumbuzi Papo Kwa Papo Kwa Zile Zilizokuwa Zipo Ktk Uwezo Wake,Lakini Pia Mwenyekiti Huyo Wa Vijana Aliwakalia Kooni Viongozi Wa Soko Ilo Kwa Kuwataka Wakakae Chini Upya Na Kuangalia Namna Ya Kuwapunguzia Kero Za Tozo Na Ushuru Uliokithiri Haswa Ktk Swala Zima La Tozo Za Usafi Wa Soko Hilo. Mwenyekiti Huyo Wa Vijana Pia Amewataka Wananchi Na Wafanyabiashara Wa Soko Ilo Kutokuogopa Na Kutishwa Na Kelele Zinazopigwa Na Wapinzani Wa Serikali Ya CCM Ktk Mkoa Huo Kwamba Eti Wafanyabiashara Hao Watahama Ktk Eneo Hilo Huku Mwenyekiti Huyo Wa Vijana Akiwajibu Na Kuwa...

AWESO AKAGUA MRADI WA MAJI SHINYANGA.

Picha
Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe Juma Aweso akijaribu kuendesha baiskeli yenye madumu ya maji ili kujionea kwa vitendo namna ambavyo wananchi wanakumbwa na adha hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Shinyanga Jana 10 Januari 2018. Baadhi ya wananchi wakizungumza na  Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe Juma Aweso kufikisha malalamiko yao kuhusu kadhia ya maji  wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Shinyanga Jana 10 Januari 2018. Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe Juma Aweso akizungumza jambo wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Shinyanga kukagua miradi ya maji Jana 10 Januari 2018 akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg  Baraka Shemahonge Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe Juma Aweso akifurahi na wanafunzi wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Shinyanga Jana 9 Januari 2018 Na Mathias Canal, WazoHuru Blog Naibu Waziri wa Wizara ya ...

Picha : BASI LA ALLYS LAPINDUKA, LAUA NA KUJERUHI WATU 25 SHINYANGA

Picha
Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Lucas Maganga (25) mkazi wa Shinyanga mjini amefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya Basi la Allys lenye namba za usajili T. 979 CDH lililokuwa linatoka Ushirombo kwenda Bariadi mkoani Simiyu kupasuka gurudumu na kupinduka eneo la Maganzo mkoani Shinyanga.  Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Septemba 25,2017 majira ya saa nne asubuhi.  Mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia Malunde1 blog kuwa gurudumu la mbele la basi hilo lilipasuka na kwamba dereva wake Salumu Mseke alikuwa akiendesha kwa mkono mmoja huku akiongea na simu ya mkononi. Wamesema basi hilo lina uwezo wa kubeba abiria 50,lakini waliokuwa ndani ya basi ni zaidi ya 70 na dereva alikimbia baada ya kusababisha ajali hiyo. Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.  Basi la Allys Sports likiwa kimepinduka Tairi likiwa limepasuka Uokoaji ukiendelea

MAGUFULI KUONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA - NEC KWA SIKU MBILI DAR

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Taifa, anatarajia kuongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam, Septemba 30 hadi Oktoba 1, 2017. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Septemba 24 na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole ameeleza kuwa, Kamati kuu ya Halmashauri ya Taifa (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) vinatarajia kuketi Jijini Dar e Salaam kwa nyakati tofauti.

MBUNGE WA CHADEMA JOSHUA NASSARI "NIPO TAYARI KUJIUZULU UBUNGE..NINA USHAHIDI MADIWANI KUPEWA RUSHWA KUJIUZULU"

Picha
Mbunge wa Chadema wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ameweka rehani ubunge wake  baada ya Rais John Magufuli kumpokea aliyekuwa diwani wa chama hicho aliyejiuzulu akisema ni kwa sababu ya kuunga mkono juhudi za Rais. Nassari amedai ana ushahidi wa kielektroniki unaoonyesha madiwani hao walivyopewa rushwa ili wajiuzulu nafasi zao. Hata hivyo, diwani wa Kata ya Kimandolu, Mchungaji Rayson Ngowi ambaye amepokewa na Rais Magufuli juzi  baada ya kujiuzulu Chadema akizungumzia tuhuma hizo alisema madai hayo hayana ukweli wowote na kama Nassari ana ushahidi ni vyema angeutoa hadharani. Ngowi aliwashauri Chadema mkoani Arusha watatue matatizo yaliyopo ndani ya chama hicho na wasitafute visingizio kwa kuwa yeye ameamua kujiuzulu kwa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli na hajapewa rushwa yoyote. Diwani mwingine aliyejiengua katika chama hicho wa Kata ya Muriet, Credo Kifukwe alisema hakuna chochote alichopewa kama rushwa kwa lengo la kujiuzulu, akims...