Ujenzi wa kituo cha Afya Kirando wapamba moto...
Mkuu wa wilaya Nkasi Mh.Said Mtanda amekagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya kirando kinachokadiriwa kukamilika kwa gharama ya Sh.milion700 ikiwa ni sambamba na Ununuzi wa Vifaa tiba.Katika ziara hiyo mkuu wa wilaya aliongozana na Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mh.Ally kessy kufuatilia hali ya ujenzi wa kituo hicho.Ikiwa ni siku chache zilizopita tangu wananchi wa mji wa Kirando wajitokeze kwenye Songambele ya Ujenzi wa kituo hicho katika hatua ya awali(msingi) ili kubana matumizi ya fedha na kuongeza jengo la kuhifadhia maiti.
Maoni
Chapisha Maoni