MKUU wa mkoa Rukwa Zellote Stephen amewataka watumishi wa serikali kutoa huduma sahihi kwa Wananchi
MKUU wa mkoa
Rukwa Zellote Stephen amewataka watumishi wa serikali kutoa huduma sahihi kwa
Wananchi wanaowahudumia na si kuzitumia ofisi za serikali kuwa ni sehemu ya
biashara na kinyume na misingi ya kazi zao
Amedai kuwa
utumishi wa umma una maadilio yake kiutendaji na lengo kubwa ni kumuhudumia
Mwananchi hivyo huduma hizo zitolewe kwa kufuata kanuni na misingi ya kazi
husika na si kutoa hudiuma hizo kwa upendeleo na rushwa.
Akizungumza
na watumishi wa serikali wanaofanya kazi makao makuu ya halmashauri ya wilaya
mkuu huyo wa mkoa amedai kuwa ili kuweza
kuendana na serikali ya awamu ya tano ni lazima watumishi wa Umma kufanya kazi
zao kwa kufiuata misingi kinyume cha hapo ni kufukuzwa kazi na hata kufikishwa
mahakamani
Mkuu huyo wa
mkoa pia ameitumia siku ya leo kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ambazo
zimekosa ufumbuzi muda mrefu
Mhe,zellote amekamilisha ziara ya siku tatu
wilayani Nkasi ambapo ameweza kukagua na kuhamasisha shughuli mbalimbali za
maendeleo
Maoni
Chapisha Maoni