amejinyonga hadi kufa kwa kutumia nguo ngumu



KIJANA mmoja aliyetambulika kwa jina la Venance Kuchangwa(24) mkazi wa kijiji cha Miyombo  kata ya Mashete  wilayani Nkasi amejinyonga hadi kufa kwa kutumia nguo ngumu.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo afisa mtendaji  wa kata ya Mashete Cresence Paulo  alisema kuwa kijana huyo alikutwa amekufa akiwa amejitundika juu ya mti jana majira ya saa tisa alasiri.
Amesema kijana huyo alijinyonga kutokana na ugumu wa maisha baada ya kuacha shule kidato cha tatu na kwenda kufanya kazi za kubeba mizigo ambazo hazikuweza kubadilisha maisha yake.
Alifafanua kuwa  licha ya kijana huyo kutotoa maelezo yoyote yaliyotokana na kifo chake ni kuwa amekuwa akilalamikia ugumu wa maisha baada ya kuacha shule na kwenda kuoa mke huku wazazi wake nao wakionyesha kumtegemea
Hivyo kifo hicho  kimehusishwa moja kwa moja na ugumu  huo wa maisha kutokana na malalamiko ya mara kwa mara al;iyokuwa akiyazungumza kutokana na ugumu wa maisha uliokuwa ukimkabili hasa baada ya kuoa
Sikamba amedai kuwa kilichopelekea ugumu zaidi wa maisha kwa kijana huyo ni kwa kutegemea kazi moja tu ya kubeba mizigo na kuacha kujishughulishja na kilimo kitu ambacho ingekuwa ni ngumu kwake kutoka kimaisha licha ya wao kumshauri  kujishirikisha na suala zima la kilimo pia
Polisi baada ya kuufanyia uchunguzi mwili huo wa marehemu ndugu waliruhusiwa kuendelea na shughuli za mazishi ambapo jana hiyo hiyo mazishi yalifanyika

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HUYU NDIO DJ MARK WA 92.2FM SUMBAWANGA.....