Machapisho

Diamond atua Afrika Kusini kwa Zari

Picha
Ikiwa zimepita siku nne tangu mwanamuziki Diamond Platnumz akiri kumsaliti mpenzi wake Zari, hatimaye ametua nyumbani kwa mwanamke huyo nchini Afrika Kusini.  Leo saa 5.40 asubuhi mwanamuziki huyo aliposti video katika mtandao inayomuonyesha  akicheza na mtoto  wake wa kwanza, Latifah huku kwa mbali ikisikika sauti ya Zari. Dada wa mwanamuziki huyo, Esmah Khan aliposti video hiyo katika mtandao wa Instagram: “Tuko na  Tiffah na mamy  tunaita raha ya mtoto apewe mapenzi kwa baba na mama jamani.”  Leo ilikuwa siku muhimu kwa  Zari kwani anasherehekea  siku yake ya kuzaliwa.

JPM amwaga ajira 3,000 JWTZ

Picha
Rais John Magufuli ametangaza kutoa nafasi 3,000 kwa vijana waliopitia mafunzo ya ukakamavu kujiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Akizungumza baada ya kuwatunuku  nishani ya Luteni Usu maofisa 422  wa jeshi, Magufuli amesema lengo la kutoa nafasi hizo ni kuhakikisha jeshi linakuwa na askari wa kutosha. “Jeshi haliwezi kuwa na maofisa tu, tutaongeza na askari wa kawaida, wengi watakaopata nafasi hizi nataka wawe wamepitia JKT, tunataka tujenge jeshi la kisasa.” Rais Magufuli amewataka Watanzania kutoa ushirikiano kwa jeshi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili viendelee kufanya kazi yao kwa ufanisi, amani na utulivu viendelee kutawala nchini.

Picha 20 : RC SHINYANGA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI 'SHINYANGA MPYA,MTI KWANZA'

Picha
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akizindua kampeni ya upandaji miti ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ leo Septemba 23,2017- Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog ***** Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack amezindua kampeni ya upandaji miti katika wilaya ya Shinyanga yenye kauli mbiu ya  ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’  ili kuboresha mazingira  Shinyanga na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha jangwa.  Kampeni hiyo inayoratibiwa na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, imezinduliwa leo Jumamosi Septemba 23,2017 katika manispaa ya Shinyanga ,kwa lengo la kuboresha mazingira ya mji wa Shinyanga,maeneo ya taasisi,maeneo ya wazi,maeneo yanayozunguka kaya,kandokando ya barabara na sehemu zingine ambazo hazina miti.  Akizungumza wakati wa kuzindua kampeni hiyo,Telack alisema kutokana na mvua haba katika mkoa wa Shinyanga, kumekuwepo na mabadiliko ya tabia nchi hali inayosababisha kuwepo na hali ya jangwa.  Telack al...

MSHINDI WA TIGO FIESTA SUPA NYOTA 2017 APATIKANA JIJINI MWANZA

Picha
Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 toka Mwanza, Fatuma Msafiri akiimba wakati wa kumtafuta mkali wa kipaji cha kuimba jijini Mwanza  Msanii Chipukizi Lusinde Michael a.k.a Real Da Best akionesha umahiri wake wa kufoka foka kwenye mchuano wa kusaka kipaji cha Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 jijini Mwanza Top 2 wakisubiri kutajwa kwa mshindi kati yao.  Majaji wakijadiliana jambo. Wasanii walioingia Top 4 wakisubiri mchujo wa kuingia top 2.  Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 kutoka Mwanza akibubujikwa na machozi ya furaha mara baada ya kutangazwa kushinda shindano la kusaka vipaji vya kuimba Supa Nyota msimu huu wa Tigo Fiesta 2017, Pembeni mshindi wa pili Lusinde Michael a.k.a Real Da Best.  Sehemu ya umati uliojitokeza kushiriki Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 jijini Mwanza.  Majaji wakiongozwa na Nickson wakiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 toka Mwanza Fatuma Msafiri. TAGS:

VIJANA WAWILI WATUPWA JELA MAISHA KWA KUMBAKA MKE WA MTU KWA ZAMU

Picha
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imewahukumu kifungo cha maisha jela washtakiwa wawili baada ya kupatikana na hatia katika makosa matatu ya kubaka kwa zamu, kulawiti na kujeruhi. Washtakiwa Fabian Charles (18) maarufu Kisigara na Asinani Kondo (22) wakazi wa Pugu kwa Mustafa wanadaiwa kumbaka, kumlawiti na kumjeruhi kwa kumchoma na bomba la pikipiki mwanamke mwenye miaka 26 mbele ya mume wake walipokuwa wakitoka matembezi. Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 22 mwaka 2015 katika eneo la Pugu wilayani Ilala. Hukumu hiyo imetolewa jana Ijumaa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan aliyesema wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo upande wa mashitaka ulipeleka mashahidi wanne waliothibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka. Hakimu amesema katika kosa la kwanza ambalo ni kubaka kwa zamu washtakiwa watatumikia kifungo cha maisha jela. Kwa shtaka la pili la kulawiti washtakiwa kwa pamoja wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela. Kisigara ambaye kati...

JWTZ YATOA TAARIFA KUHUSU MWANAJESHI ALIYEUAWA CONGO

Picha
Taarifa kwa Vyombo vya Habari Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa mwili wa marehemu Praiveti Mussa Jumanne Muryery ambaye ameuawa nchini DRC akiwa katika jukumu la Ulinzi wa Amani, utaagwa kwa heshima tarehe 25 Septemba 2017 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo kuanzia saa 2:00 asubuhi. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Florens M. Turuka ataongoza katika kuuaga mwili wa Marehemu. Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi Amin. Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano 22 Septemba, 2017.

MSEMAJI WA SERIKALI AWAJIBU CHADEMA: WAMEKUFA WATU WANGAPI KIBITI HATUKUITA WAZUNGU?

Picha
Baada ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusikika wakidai vyombo vya usalama kutoka nje ya nchi vije kufanya uchunguzi wa shambulio la MbungeTundu Lissu, Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbaas amefunguka na kuhoji watu wangapi wamekufa na wazungu hawakuja. Kupitia ukurasa wake wa twitter Dkt. Abbas amehoji kwa kuandika "Waje wazungu? Wamekufa watu wangapi Kibiti hatukuita wazungu?Lakini hatujui pia hata hao wazungu kwao makosa ya jinai pia yamewazidi nguvu? Hata hivyo Dkt Abbas ameongeza kwamba tabia ya kutuhumiana kunapotokea kosa la jinai ambalo limetendwa kwa mtu yoyote au mwanasiasa siyo vizuri kwani kufanya hivyo kunakufanya uwe mshukiwa namba moja wa tukio. Ameongeza kwamba kwamba ni "busara vyombo vya dola vikaachwa vifanye kazi yake kwanza na siyo kutuhumu". Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia viongozi wake wamekuwa wakitaka serikali iruhusu vyombo vya kimataifa waje nchini kufanya uchunguzi juu y...