TAMASHA LA MUZIKI NA UTAMADUNI WILAYA YA NKASI 19-20/2017.



Mkuu wa wilaya ya Nkasi Said Mohamed Mtanda ameungana na wasanii na viongozi mbalimbali
Katika Tamasha lililofanyika siku ya Jumamosi na Jumapili ya Tarehe 19 na 20 ili kuunga mkono
Kampeni ya Kuzuia na kupambana na Madawa ya kulevya hivyo aliwataka vijana kuepukana na
tabia ya uvutaji bangi na matumizi ya pombe kali yaani Viroba.Tamasha hilo pia lilipambwa na Ngoma za asili ikiwemo kikundi cha NkomanChindo msanii Robby GUITER na Young Steve msanii
wa Hip Hop toka Sumbawanga manispaa.Wakazi wengi wa Namanyere walijitokeza na kumpongeza
mkuu wa wilaya kwa kujali sanaa ndani ya wilaya.Pia yalifanyika mashindano ya kuwapata wasanii
wenye uwezo wa kuimba ambapo watapata fursa ya kwenda jijini Dar es saalam kufanyiwa majaribio
msanii Jozedah ndio aliyeibuka kinara akifuatiwa na Kisu Mofire na Paul wa milazo.
huku viongozi mbalimbali wa kiserikali wakisindiza tamasha hilo.
Tamasha hilo lilienda sambamba na Tendo la uchangiaji damu salama, upimaji wa VVU kwa hiari.

imehaririwa na MacTz

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HUYU NDIO DJ MARK WA 92.2FM SUMBAWANGA.....