Machapisho

MSHINDI WA TIGO FIESTA SUPA NYOTA 2017 APATIKANA JIJINI MWANZA

Picha
Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 toka Mwanza, Fatuma Msafiri akiimba wakati wa kumtafuta mkali wa kipaji cha kuimba jijini Mwanza  Msanii Chipukizi Lusinde Michael a.k.a Real Da Best akionesha umahiri wake wa kufoka foka kwenye mchuano wa kusaka kipaji cha Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 jijini Mwanza Top 2 wakisubiri kutajwa kwa mshindi kati yao.  Majaji wakijadiliana jambo. Wasanii walioingia Top 4 wakisubiri mchujo wa kuingia top 2.  Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 kutoka Mwanza akibubujikwa na machozi ya furaha mara baada ya kutangazwa kushinda shindano la kusaka vipaji vya kuimba Supa Nyota msimu huu wa Tigo Fiesta 2017, Pembeni mshindi wa pili Lusinde Michael a.k.a Real Da Best.  Sehemu ya umati uliojitokeza kushiriki Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 jijini Mwanza.  Majaji wakiongozwa na Nickson wakiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2017 toka Mwanza Fatuma Msafiri. TAGS:

VIJANA WAWILI WATUPWA JELA MAISHA KWA KUMBAKA MKE WA MTU KWA ZAMU

Picha
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imewahukumu kifungo cha maisha jela washtakiwa wawili baada ya kupatikana na hatia katika makosa matatu ya kubaka kwa zamu, kulawiti na kujeruhi. Washtakiwa Fabian Charles (18) maarufu Kisigara na Asinani Kondo (22) wakazi wa Pugu kwa Mustafa wanadaiwa kumbaka, kumlawiti na kumjeruhi kwa kumchoma na bomba la pikipiki mwanamke mwenye miaka 26 mbele ya mume wake walipokuwa wakitoka matembezi. Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 22 mwaka 2015 katika eneo la Pugu wilayani Ilala. Hukumu hiyo imetolewa jana Ijumaa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan aliyesema wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo upande wa mashitaka ulipeleka mashahidi wanne waliothibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka. Hakimu amesema katika kosa la kwanza ambalo ni kubaka kwa zamu washtakiwa watatumikia kifungo cha maisha jela. Kwa shtaka la pili la kulawiti washtakiwa kwa pamoja wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela. Kisigara ambaye kati...

JWTZ YATOA TAARIFA KUHUSU MWANAJESHI ALIYEUAWA CONGO

Picha
Taarifa kwa Vyombo vya Habari Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa mwili wa marehemu Praiveti Mussa Jumanne Muryery ambaye ameuawa nchini DRC akiwa katika jukumu la Ulinzi wa Amani, utaagwa kwa heshima tarehe 25 Septemba 2017 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo kuanzia saa 2:00 asubuhi. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Florens M. Turuka ataongoza katika kuuaga mwili wa Marehemu. Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi Amin. Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano 22 Septemba, 2017.

MSEMAJI WA SERIKALI AWAJIBU CHADEMA: WAMEKUFA WATU WANGAPI KIBITI HATUKUITA WAZUNGU?

Picha
Baada ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusikika wakidai vyombo vya usalama kutoka nje ya nchi vije kufanya uchunguzi wa shambulio la MbungeTundu Lissu, Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbaas amefunguka na kuhoji watu wangapi wamekufa na wazungu hawakuja. Kupitia ukurasa wake wa twitter Dkt. Abbas amehoji kwa kuandika "Waje wazungu? Wamekufa watu wangapi Kibiti hatukuita wazungu?Lakini hatujui pia hata hao wazungu kwao makosa ya jinai pia yamewazidi nguvu? Hata hivyo Dkt Abbas ameongeza kwamba tabia ya kutuhumiana kunapotokea kosa la jinai ambalo limetendwa kwa mtu yoyote au mwanasiasa siyo vizuri kwani kufanya hivyo kunakufanya uwe mshukiwa namba moja wa tukio. Ameongeza kwamba kwamba ni "busara vyombo vya dola vikaachwa vifanye kazi yake kwanza na siyo kutuhumu". Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia viongozi wake wamekuwa wakitaka serikali iruhusu vyombo vya kimataifa waje nchini kufanya uchunguzi juu y...

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 23,2017 - NDANI NA NJE YA TANZANIA

Picha
Magazetini leo Jumamosi Septemba 23,2017

WAZIRI CHARLES MWIJAGE AFUNGUA TAWI LA KAMPUNI YA MABATI ALAF DODOMA

Picha
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage  akifungua tawi la kampuni ya mabati ya ALAF  Dodoma. Kushoto ni meneja mkuu Upauaji  (roofing) wa Kampuni ya mabati  ALAF, Dipti Mohanty  akishuhudia ufunguzi huo. *** WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage Septemba 9, 2017 alifungua tawi la Kiwanda cha mabati ALAF katika mkoa wa Dodoma eneo la Kizota kitalu namba 148. Kufunguliwa kwa tawi hili katika mkoa wa Dodoma ni  kutokana na maamuzi ya serikali  kuamia makao makuu ya nchi mkoani Dodoma kwa vitendo  na  kuunga mkono kauli mbiu ya Mheshimiwa  Rais John Magufuli katika  “ USHIRIKI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA TAIFA”. Kufunguliwa kwa tawi hili  kutaimarisha maendeleo ya mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani. Wateja kutoka Dodoma na Singida  sasa wataweza  kupata suluhisho la mahitaji ya bidhaa za uezekaji kutola ALAF. Tunauza...