WAZIRI CHARLES MWIJAGE AFUNGUA TAWI LA KAMPUNI YA MABATI ALAF DODOMA
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage akifungua tawi la kampuni ya mabati ya ALAF Dodoma. Kushoto ni meneja mkuu Upauaji (roofing) wa Kampuni ya mabati ALAF, Dipti Mohanty akishuhudia ufunguzi huo. *** WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage Septemba 9, 2017 alifungua tawi la Kiwanda cha mabati ALAF katika mkoa wa Dodoma eneo la Kizota kitalu namba 148. Kufunguliwa kwa tawi hili katika mkoa wa Dodoma ni kutokana na maamuzi ya serikali kuamia makao makuu ya nchi mkoani Dodoma kwa vitendo na kuunga mkono kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais John Magufuli katika “ USHIRIKI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA TAIFA”. Kufunguliwa kwa tawi hili kutaimarisha maendeleo ya mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani. Wateja kutoka Dodoma na Singida sasa wataweza kupata suluhisho la mahitaji ya bidhaa za uezekaji kutola ALAF. Tunauza...